Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Nuru inapoiangazia dunia, huwaangazia viumbe vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, viumbe vyenye uhai, hao hufurahia nuru hiyo kwa kuruka ruka na kucheza kufurahia nuru hiyo.
Kila ifikapo asubuhi na mapema, utasikia sauti na milio ya ndege wa angani, wanyama wa kufuga na waishio mwituni, milio na sauti za viumbe hao wakati mwingine kuashiria kuwa kumekucha ili waendelee kufurahia nuru inayowanaagazia kwa manufaa ya maisha yao.
Wanadamu nao wakiwa kama viumbe hai wengine, huanza kujiandaa asubuhi na mapema kuelekea huku na kule kutafuta riziki ya kila siku ili maisha yao yaendelee kusonga mbele baada ya nuru kuwangazia.