Baada ya msanii wa Bongo Flava, Linah Sanga kupoteza akaunti yake ya Instagram yenye zaidi ya followers milioni 1.3, pamekuwepo na maneno mengi. Wapo wanaosema kuwa Linah ameiuza na kufungua nyingine Linah.

“Kwanza hadi sasa hivi bado naendelea na mipango ya kurudisha hiyo akaunti yangu na maendeleo naona ni mazuri karibia asilimia 90, namuomba Mungu tu ili irudi,” ameiambia Bongo5.
“Pia naawaambia mashabiki wangu kwa sasa sina akaunti yoyote ya Instagram kwahiyo wawe makini sana maana kuna watu wamekuwa wakiniambia kuwa nimefungua akaunti mpya, aisee hapana sijafungua kabisa wawe tu makini na hao ambao wanajifanya ndio mimi,” ameonya Linah.
Pia amesema ameathirika vikali kutokana na kuipoteza akaunti yake hiyo.
“Imeniathiri kweli kwakweli hasa kwa upande wa mashabiki wangu ambao wamekuwa wakitaka kujua kuna vitu hapa katikati vimetokea ambavyo mashabiki wangu walitakiwa kufahamu, lakini wameshindwa kwa kweli na wengine kujua ratiba zangu za show kwakweli imeniathiri kiasi chake.”
Kuhusu tetesi za kuwa ameiuza, Linah amesema:
“Yaani sidhani kama naweza kufanya hivyo nikauze akaunti yangu wakati mimi mwenyewe biashara. Unajua kuna watu wanapenda kukurupuka na kuanza kuongea vitu wasivyovijua na hiyo imeniuma sana kwakweli watu kuongea ujinga, hawajui nimeumia kiasi gani yaani hadi nahisi nimekonda siyo vizuri watu waongee vitu ambavyo hawana uhakika navyo.”