Kwa msanii hakuna kinachouma kama pale anapotoa nyimbo nyingi mfululizo halafu zikaishia kutambulishwa tu redioni.
![haroun](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2016/07/xharoun.jpg.pagespeed.ic.Br9CODm6wv.jpg)
Inspekta Haroun anadai kuwa alianza kufikiria biashara nyingine ya kufanya baada ya kutoa nyimbo takriban 20 na zote zikapotea hivi hivi.
“Nilitoa karibu track 20, halafu zote hazikupata airtime kwasababu kuliingia kavurugu fulani kwenye hizi media zetu kukawepo na kitu wanaita promo,” Inspekta alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Kwahiyo nyimbo zangu ambazo nilikuwa nazifanya na nikaziamini kama ambavyo style watu walikuwa wanazipenda sana hazikuwahi kupewa nafasi na hazikumrudisha Inspekta yule watu wanamhitaji,” aliongeza.
Pamoja na kurekodi nyimbo kwa kufuata ushauri aliokuwa akipewa na watu wa redio, bado aliendelea kubaniwa licha ya mashabiki kuzipenda ngoma zake.
“Iliniumiza lakini baadaye familia yangu ikanifanyia counselling nikaona mashabiki wangu wananihitaji kwahiyo niliendelea na sanaa.”
Bongo 5