Baada ya Serikali ya awamu ya 5 kutangaza kuhamia Dododma kutekeleza Adhma ya waasisi wa Taifa letu,Naibu Waziri wa Ajira,Kazi na Maendeleo ya vijana Mhe.Anthony Mavunde ambaye pia ni mbunge wa Dodoma Mjini leo Amekagua Ujenzi wa barabara ya Sango Soko kuu Majengo ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami na kuwekwa taa za barabarani.Barabara hii ilikuwa korofi na haikuwa rafiki kwa watumiaji kutokana na kuharibiwa sana na mvua.
Pamoja na barabara hii pia zitajengwa kwa kiwango cha lami barabara za kutoka Amani shule ya msingi itakayounga na Iringa Road,Majengo sokoni mpaka Hazina,Uhindini na Uzunguni mtaa wa Biring kwani pia ilikuwa Ahadi yake kipindi cha kampeni ikiwa ni kuhakikisha miundombinu yote ya Dodoma inakuwa imara kabla ya Serikali kuhamishia Shughuli zake mkoani Humo.