Quantcast
Channel: MC DR CHENI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

MSIBA: Aliyekuwa Rais wa Z’bar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi afariki dunia -

$
0
0


Taarifa tulizozipata hivi punde ni kuwa Rais Mstaafu wa zanzibar wa awamu ya pili Mzee ABOUD JUMBE MWINYI amefariki dunia mchana huu nyumbani kwake Kigamboni.
Taarifa za awali zinasema alikuwa ameugua kwa muda mrefu.
Taarifa zaidi za msiba huo zitakujia hivi punde. 

#‎Kauli_ya_Zitto_Kabwe‬.
"Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ametangulia mbele ya Haki. Inna lillah waina ilaih raajiun.

Mzee Jumbe atakumbukwa katika historia ya Tanzania Kama Kiongozi aliyeamini na kusimamia anachoamini bila kujali madhara yake. Alipoteza nafasi zake za Uongozi Kwa sababu ya msimamo wake kuhusu muundo wa Muungano kutoka Serikali 2 kwenda Serikali 3.

Mzee Jumbe ameacha maandiko kupitia kitabu chake cha The Partnership ambacho ndugu yetu Ali Ally Saleh ' Alberto ' alipata heshima ya kukifasiri.

Pia Mzee Jumbe ameacha ' memoir ' yake ambayo ninaamini walioachiwa sasa wataweza kuitoa ili dunia ipate kujua mengi ambayo labda hatujui kuhusu Nchi yetu.

Hivi hapa Tanzania kuna Hata barabara yenye jina la Aboud Jumbe Mwinyi? Daraja? Nchi hii wakubwa wakigombana huwa hawasameheani?

Wazanzibari wanaweza kutumia msiba wa Mzee Jumbe kujenga maridhiano na kuanza kujenga Zanzibar kwa pamoja?"



Unaweza kutazama historia yake kidogo hapa

Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa rais wa pili wa Zanzibar toka mwaka1972 hadi 1984 alipojiuzulu. 

Aboud Jumbe alizaliwa mwaka1920 huko kisiwani Zanzibar ( Tanzania ).




Alitanguliwa na Abeid Amani KarumeMakamu wa Rais wa Tanzania1972-1984 akafuatiwa na
Ali Hassan Mwinyi




Mwinyi Aboud Jumbe (born 14 June 1920) was a politician in Zanzibar. He held several positions, including the second president of Zanzibar


chairman of the Revolutionary Council, Vice-President of the Union, and the vice-chairman of the Chama Cha Mapinduzi (CCM) party.

Jumbe served as president of Zanzibar from 11 April 1972 until 30 January 1984. He succeeded Abeid Karume as president, following Karume's assassination on April 7, 1972. He was initially elected by the Revolutionary Council as a part of the Afro-Shirazi Party (ASP). While he was in office, in 1977, the two ruling parties of Tanzania merged. In particular, the ASP and the Tanganyika African National Union (TANU), merged to create Tanzania's ruling party, the CCM.


In 1979, Jumbe introduced the first post-revolutionconstitution of Zanzibar. This separated the powers of theRevolutionary Council and the House of Representatives. Furthermore, the new constitution established elections byuniversal suffrage, instead of being elected by the Revolutionary Council.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>