Kadhalika, wabunge wameunga mkono juhudi za serikali na wameridhia kukatwa posho ya siku moja ili kuchangia kusaidia maafa yao.
Hatua hiyo inafuatia muongozo wa mbunge wa Mlalo CCM, Rashid Shangazi aliyeomba kiti kutoa muongozo ili wabunge watoe fedha hizo kama sehemu ya kuomboleza pamoja na waathirika.
Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa pande zote bila kuangalia itikadi zao.
Hata hivyo, Mbunge wa Tarime vijijini Chadema John Heche alisema chama chake kilishatoa Sh 100,000 kila mbunge lakini kufuatia hoja hiyo na wao wapo tayari kuchangia posho zao.