Raymond, Vanessa Mdee na Yamoto Band wameongezeka kwenye nomination za tuzo za MTV MAMA 2016. Diamond na Alikiba ambao walikuwa wametajwa awali, wameongezeka tena kipengele kimoja kimoja.
![tuzo](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2016/10/xtUZO.jpg.pagespeed.ic.-tUciJv578.jpg)
Raymond ametajwa kuwania kipengele cha Best Breakthrough Act, Vanessa Mdee – Best Female, Yamoto Band – Lister’s Choice Awards, Diamond – Artist of the Year na Alikiba na Sauti Sol – Song of the Year.
Tuzo hizo zitafanyika Oktoba 22 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Diamond na Alikiba ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza.