Quantcast
Channel: MC DR CHENI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Wasanii wa filamu watakiwa kutunga filamu zenye maadili ya kitanzania

$
0
0
Waziri wa habari, sanaa, utamaduni, michezo,Nape Nnauye amewataka wasanii wa filamu nchini Tanzania kutunga filamu zenye kufunza maadili ya kitanzania ambayo yatasaidia kuielimisha jamii.
nape
Wasanii hao walikusanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mawazo yao yatakayosaidia kutengeza sera mpya ya filamu nchini.
“Na mimi ninatamani filamu yetu, tasnia ya filamu, pamoja na ajira na uchumi na mambo mengine, mfanye kazi ya kututengenezea watanzania tunaowataka, kwamba mtu akiangalia filamu, kijana akiangalia filamu anatengenezwa na ile filamu kuwa mtanzania tunayemtaka,” alisema Nape.
BY: EMMY MWAIPOPO

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>