![](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2016/10/20161005_122529.jpg?resize=660%2C400)
Shirikisho la soka Tanzania TFF leo October 5 2016 kupitia kwa afisa habari wake Alfred Lucas imetangaza maamuzi yaliofikiwa na kamati kuhusiana na mchezo wa Simba naYanga uliochezwa October 1 2016 na kumalizika kwa sare ya goli 1-1 na mashabiki waSimba kuvunja viti kutokana na refa Martin Saanya kukubali goli la Amissi Tambwealiyekuwa amehushika mpira.
TFF imetoa adhabu kadhaa kuhusiana na matukio mbalimbali sambamba na kuipiga fainiAzam FC kwa kucheza mechi ikiwa imevaa jezi zenye logo ya mdhamini upande mmoja, hata hivyo refa aliyefungiwa ni Ahmed Seif kwa kushindwa kumudu mechi ya African Lyon na Mbao FC, hivyo amefungiwa miezi sita.
![qt](http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2016/10/qt.png?resize=571%2C370)
Kwa upande wa Martin Saanya TFF imetangaza kuwa imefuta kadi nyekundu aliyomuonesha Jonas Mkude wakati wa mechi ya Yanga na Simba, lakini refa huyo anachunguzwa kufuatia uchezeshaji wake aliouonesha katika mechi hiyo.