Msanii mkongwe wa filamu nchini Bi Hindu amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa tasnia hiyo nchini hawapendani.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Uhondo cha EFM, amekiambia kipindi hicho kuwa wasanii wengi hawapendani na wamekuwa wakichukia mafanikio ya wenzao.
“Wasanii wa Bongo movie hatupendani, tupunguze roho mbaya. Wenzetu wakitaka kufanya kitu tuwape ushirikiano,” amesema Bi Hindu.
Mkongwe huyo wa filamu aliongeza kwa kutania kwa kusema kuwa na yeye akipata jina basi watamkoma.