![](http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2016/11/mnny.png?resize=660%2C400)
November 12 2016 yamefanyika mazishi ya Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel John Sitta aliyefariki dunia November 7 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.
Mazishi hayo yamefanyika Urambo Tabora kwenye eneo la makaburi ya ukoo wa Sitta ambayo yapo takribani km 2 kutoka nyumbani kwake.
#MillardAyoUPDATES Mazishi ya Spika mstaafu Samuel Sitta ambaye anazikwa katika makaburi ya familia ya ukoo wa Sitta, Urambo Tabora
#MillardAyoUPDATES Safari ya kuelekea eneo la makaburi ambapo mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta utazikwa
#MillardAyoUPDATES Waziri Nape Nnauye akiongea machache wakati wa kuuaga mwili wa Samuel Sitta Urambo Tabora
#MillardAyoUPDATES Ibada ya kumuombea Mzee Sitta imeanza muda huu viwanja vya shule ya msingi Urambo, mazishi yatafanyika majira ya saa nane