
Filamu hiyo imepangwa kuachiwa siku aliyozaliwa rapper huyo Juni 16, 2017. Kwenye filamu hiyo Demetrius Shipp ameigiza kama Tupac huku Danai Gurira akiigiza nafasi ya Afeni Shakur ambaye ni mama mzazi wa rapper huyo ambaye alifariki mwezi Mei, mwaka huu kwa tatizo la mshtuko wa moyo.
Wakati huo huo Jamal Woolard ameigiza kama The Notorious B.I.G, Dominic L. Santana ameigiza kama Suge Knight.
Tupac alifariki dunia Septemba 13, 1996 kwa kupigwa risasi.