![](http://www.perfect255.com/wp-content/uploads/2016/11/princeamigo-20161109-0001-696x461.jpg)
Msanii wa Jahazi Morden Taarabu Amigo Prince amesema baada ya maamuuzi ya Mzee Yusuph kuachana na muziki na kumrudia Mungu wasanii 15 akiwemo Khadija Yusuph wameihama bendi.
Amigo
Akipiga story ndani ya eNews Amigo amesema baada ya Mzee kuacha muziki wasanii walianza kuyumba kiuchumi na baadhi ya wasanii kuona maisha yao yatakuwa magumu na kuanza kuhama mpaka sasa wamebaki wasanii 4 kwenye bendi ya Jahazi.
Pia Amigo amesema bendi ya Jahazi ilikuwa chini ya Hamisi Doa baada ya Mzee kuondoka lakini pia hata Khadija Yusuph alipewa kipaumbele cha kutosha na alikuwa akishirikishwa katika vitu vingi katika bendi hiyo anashangaa ni kwa nini aliamua kuondoka na kuwaacha.