Dodoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema operesheni kuhusu pombe za viroba inaendelea katika mikoa mbalimbali baada ya kupigwa marufuku Machi Mosi.
Majaliwa amesema hayo katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha kwanza tangu Serikali kuhamia mjini hapa.