Quantcast
Channel: MC DR CHENI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

HIKI NDICHO AMBACHO ANGEKIFANYA RAY KIGOSI KAMA ANGEKUA WAZIRI WA HABARI,MICHEZO NA UTAMADUNI

$
0
0
Habari kubwa Tanzania na East Africa kwa ujumla kuanzia jana asubuhi ni kuhusu utenguzi wa baraza la mawaziri uliofanywa na Mh Raisi John Pombe Magufuli kwa kumvua uwaziri aliyekuwa waziri wa Habari,, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh Nape Moses Nnauye na kumuweka katika nafasi hiyo Mh Harison Mwakyembe.

Kitendo hicho kimewagusa wengi hasa wasanii ambao walikuwa na imani na kiongozi wao huyo Nape aliyevuliwa cheo hicho  cha Uwaziri.
Perfect255 imepiga story na muigizaji Vicent Kigosi (Ray) na amefunguka kuwa endapo yeye angepewa nafasi hiyo ya uwaziri ni sekta gani angeanza kuishughulikia katika sanaa.
“Mimi ningekuwa waziri wa michezo ningesema kwamba tuweze kuwachuja wasanii, kwasababu sio kila mtu ni muigizaji, sio kwasababu Ray amefanikiwa katika uigizaji basi kila mtu anataka kuwa muigizaji, hapana, kuna taratibu za kufanya. Sasa hivi kila mtu anataka kuwa muigizaji. Ukimchezesha sinema moja naye akiwa star basi anataka kuwa producer. Ni lazima kuwe na mgawanyiko wa kazi,”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>