Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

SIMBA WATOKA SARE NA MLANDEGE YA ZANZIBAR

Image may be NSFW.
Clik here to view.

Timu ya Simba SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Mlandege katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku wa leo.Mlandege ambayo ilifungwa 2-0 na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC Jumapili usiku, leo ilikuwa mwiba kwa washindi wa taji la Azam Sports Federation Cup.Simba ikicheza bila ya nyota wake wawili Emmanuel Okwi na John Bocco imeshindwa kuonesha cheche za kutikisa mabao huku ikiendelea kusuwasua katika suala umaliziaji.Simba ambayo imecheza mechi mbili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kutoka na ushindi wa goli 1-0 ikizifunga timu za Rayon Sport ya Rwanda na Mabingwa wa Zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom 1999-2ooo Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na Omog kipindi cha pili, lakini hakuwatumia kabisa Okwi na Bocco kuashiria amewapumzisha kwa ajili ya mchezo ujao Jumatano dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga kuwania Ngao ya Jamii.
Simba SC imeweka kambi kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Na watani wao wa jadi, Yanga nao wapo kisiwani Pemba kwa malengo hayo hayo.
Kikosi cha Mlandege kilikuwa; Masoud Kombo, Adam Hamad, Amir William, Abubakar Mwadini, Abubakar Omar, Hassan Ramadhani, Edwin Charles, Nicholaus Frank, Shaaban Amir, Jaffar Rajab na Mohammed Abdallah.
Simba SC; Aishi Manula, Ally Shomary, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjali, Jonas Mkude/James Kotei dk76, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk84, Mohammed Ibrahim, Laudit Mavugo/Juma Luizio dk62, Haruna Niyonzima na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Jamal Mnyate dk68.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>