Quantcast
Channel: MC DR CHENI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Kesi Inayomkabili Scopion Yashindwa Kuendelea Leo

$
0
0
Kesi Inayomkabili Scopion Shashindwa Kuendelea Leo

Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete (31) maarufu kama Scorpion, imeshindwa kuendelea baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo Flora Haule kuwa na udhuru.

Kesi hiyo inayoendeshwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ilipaswa kuendelea leo Agosti 24 kwa upande wa utetezi kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga ameiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja leo kwa ajili ya upande wa utetezi kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi, lakini Hakimu anayesikiliza shauri hilo amepata udhuru hivyo, hivyo aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Adelf Sachore ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>