Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Salum Hapi, Jumapili hii aliwaalika wasanii wa filamu na muziki katika lunch maalum na kuzungumza nao namna ya kujibrand pamoja na kukuza vipato vyao.Hapi akisalimiana na mdau wa muziki Mama Lora
Shughuli hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomon Dar es salaam ilihudhuriwa na mastaa wachache wa muziki na filamu huku wasanii wachanga wakiitikia wito kwa wingi.
Akiongea na wasanii waliojitokeza katika shughulia hiyo, Hapi amewaahidi wasanii kuandaa semina za mara kwa mara ili wajifunze kufanya sanaa kiujasiliamali.
“Nimetaka kuzungumza na wasanii kwa pamoja ili kuangalia jinsi ya kuwasaidia, sio issue za kuhusu KOSOTA au piracy za kazi zenu, nazungumza na nyie jinsi mnavyoweza kutumia majina yenu kutengeneza pesa,” alisema Hapi. “Msanii ana follows zaidi ya milioni 1 instagram lakini hana chochote, wakati kuna gazeti moja kubwa linaongoza kwa wasomaji wengi lina wasomaji 60,000 na wamiliki wake ni matajiri wakubwa, kwa nini msanii ambaye ana follows zaidi milioni 1 asiingize pesa nyingi kupitia mashabiki aliokuwa nao kwenye mitandao yake, kwa hiyo mimi nipo tayari kushirikiana na wasanii ili kuwatafutia watu waje wateme madini jinsi ya kuweza kutumia fans wako kwenye kuingiza pesa,”
Aliongeza, “Nataka wasanii wafundishwe namna ya kufanya biashara, namna ya kukopa, namna ya kupanga matumizi, wasanii wanatakiwa kujiunga katika soko la hisa, tena unaweza hata kununua hisa za laki tano na zikaweza kukupatia faidi kubwa mwisho wa mwaka, kwa hiyo nataka wasanii wafundishwe namna ya kutumia fursa hizo zote,”
Pia mkuu huyo amewataka wasanii wenye idea za kufanya vitu vikubwa kumtafuta ili aweze kuwasaidia kuwatafutia watu husika ambao wataweza kumsaidi kutimiza ndoto zao.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alipita kumsalimia DC, Ali Hapi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi akiwa na Mrisho Mpoto, Shetta pamoja Shilole
Billnas, Hapi na Shilole
Nikki wa Pili akieleza namna msanii anavyoweza kujiingia kipato kwa kutumia mitandao ya kijamii
Shilole, Shetta na Mpoto wakijadili jambo kabla ya shughuli kuanza
Zamaradi Mtetema akieleza jinsi wasanii wanavyoweza kukuza thamani zao
Billnass