Nick Gordon, ameonekana kuhusika kwenye kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, Bobbi Kristina Brown – binti wa marehemu, Whitney Houston, imeripotiwa.
![2015-02-02t203706z_1676558518_gm1e8an0slc01_rtrmadp_3_us-people-brown_80ae0bac7b6cb9532721441ae7067045-nbcnews-ux-2880-1000](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2016/09/x2015-02-02t203706z_1676558518_gm1e8an0slc01_rtrmadp_3_us-people-brown_80ae0bac7b6cb9532721441ae7067045.nbcnews-ux-2880-1000.jpg.pagespeed.ic.CpmwxN59Ub@2x.jpg)
Bobbi – mtoto pekee kwa Whitney Houston na Bobby Brown – alifariki miezi sita baada ya kuwa kwenye coma January 2015. Gordon alikuwa amepangwa kupanda kizimbani kwenye mahakama huko Fulton County, Georgia, Ijumaa hii lakini hakutokea.
Jaji wa mahakama hiyo alisema kwakuwa Gordon alishindwa kutokea mahakamani mara mbili, ni sawa na kuthibitisha kosa lake. Gordon, aliyeasiliwa na Whitney alipokuwa mdogo alikuwepo kipindi mwanamuziki huyo anazama majini na kufa bafuni na pindi mwanae anafariki katika mazingira yale yale.
Inadaiwa kuwa Gordon alimpiga Bobbi na kumpa pombe za mchanganyiko zilizopelekea kifo chake akiwa na miaka 22.