Quantcast
Channel: MC DR CHENI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

POLISI WAMPIGA RISASI NJIWA ANAYETUMIKA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA NDANI YA GEREZANI

$
0
0


 
Polisi nchini Argentina wamempiga risasi njiwa ambaye anatumiwa 
kusafirisha dawa za kulevya kupeleka kwa wafungwa gerezani. 

Njiwa huyo alionekana akiruka hadi uwanja wa gereza moja lililo mji wa Santa Rosa. 

Wakuu wa gereza hilo waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na vidonge vya dawa za kulevya. 

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC , Gazeti la Clarin lilichapisha picha ya njiwa huyo akiwa na mfuko mweupe uliokuwa na tembe 44 za dawa za kulevya. 

Magereza nchini Argentina yalitoa taarifa tangu mwaka 2013 kwamba kuna wauzaji wa dawa za kulevya waliokuwa wakiwatumia njiwa hao. 

Njiwa hao walikuwa wakisafirisha dawa hizo zaidi ya mara 15 kwa siku. Hata hivyo watu watatu walikamatwa wakiwa na njiwa hao zaidi ya 10 baada ya uchunguzi wa mwaka 2013. 

Mapema mwaka huu njiwa ambaye alikuwa na mfuko uliokuwa na tembe 178 za dawa ya kulevya alishikwa nchini Kuwait karibu na mpaka na Iraq.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>