Quantcast
Channel: MC DR CHENI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Yaliyojiri mahakamani kesi ya Manji

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake watatu wahojiwe na Polisi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amesema ameruhusu washtakiwa wahojiwe baada ya kuandikiwa barua na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum (ZCO).
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo kuwa ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.
Hakimu Shahidi alisema kuwa kama mahakama ikizuia washtakiwa hao wasiende kuhojiwa polisi itakuwa inapingana na barua ya maombi iliyowasilishwa mahakamani hapo kutoka kwa ZCO
“Nikisema mahakama izuie wasihojiwe itakuwa tunapingana nao, wakati kila siku tunapigiana kelele kila siku kuhusu upelelezi kukamilika. Hivyo sifikirii kesi hii kila siku iwe inatajwa tu.”
Hakimu Shahidi aliwakabidhi washtakiwa hao kwa Koplo Dotto ambapo amemtaka hadi kesho muda wa kazi wawe wamerudishwa mahakamani.
Chanzo: Mwananchi

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>